1. Home /
  2. Public figure /
  3. WaterFront News


Category

General Information

Phone: +1 431-338-6066



Website: www.youtube.com/channel/UCBAomio0ScZNOH5TSc5Tz8g?view_as=subscriber

Likes: 2231

Reviews

Add review



Facebook Blog

WaterFront News 23.02.2021

ALIYEGUNDUA CUT, COPY&PASTE AFARIKI Ni Larry Tesler raia wa Marekani aliyegundua programu ya kompyuta ya Cut, Copy na Paste amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74 kwa ugonjwa ambao haujawekwa wazi. Je Larry amebadilisha vipi maisha yako?

WaterFront News 03.02.2021

MAAJABU: KIBAKA ATOKOMEA NA HONGO YA TRAFIKI Huenda maafisa wa usalama barabarani maarufu kama traffic wakatafuta njia mbadala ya kuzificha fedha wanazopewa na maderefu wa magari kama hongo ya kuachiwa baada ya kukamatwa na makosa. Hii ni baada ya jamaa mmoja katika county ya Embu nchini Kenya, kuibuka msituni na kukwapua hela ya hongo aliyokuwa akipatiwa askari wa usalama barabarani na dereva wa gari dogo na kisha kupotelea kusikojulikana. ... Tukio hilo limetokea siku ya Jana Ijumatano ambapo askari ambaye jina lake limefichwa alisimamisha gari dogo la abiria na kisha kumtoza dereva faini kwa ubovu wa gari. Ilimpasa dereva kujadiliana na askari huyo ili apunguziwe adhabu na kutoa kiasi kidogo cha fedha ambayo haitaandikwa kwenye mashine na badala yake itakuwa ni hela ya huyo askari. Katika kupokea Ksh 1,500 ghafla aliibuka mtu kutoka msituni na kukwapua hiyo hela na kisha kutoweka msituni na kumwacha askari bila kujua la kufanya. Haikujulikana huyo mtu alitokea wapi kwani mahali hapo hakuna makazi ya watu yaliyo karibu.

WaterFront News 20.01.2021

HALI SI SWARI: IRAN YAKIRI KUITUNGUA NDEGE YA UKRAIN Msemaji mkuu wa jeshi la Iran amekiri kuwa ndege ya Boeing Mali ya shirika la ndege la Ukrain ilitunguliwa bahati mbaya na makombora ya Iran. Ndege hiyo ilianguka Dakika chache tu tangu kupaa mjini Tehran ikielekea Canada kupitia Kiev nchini Ukrain. Katika Picha ya video iliyochapishwa na BBC ndege hiyo Ilionekana ikigongwa na kitu cha moto mithili ya bomu kabla ya kulipuka na kuanguka. Watu wote 176 waliokuwepo ndani walif...ariki wakiwepo raia 63 wa Canada, Waingereza 4, Wairani 86, Ukrain 11 na wengine. Awali Iran ilikana kuhusika na tukio hilo lakini baada ya uchunguzi wa kina wamekiri kuwa ndege hiyo ilitunguliwa bahati mbaya baada ya kupita juu ya eneo nyeti linalokaliwa na vikosi vya Islamic Revolutionary Guard Corps kilichokuwa kikiongozwa na Generali Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani

WaterFront News 16.01.2021

TRUMP: NASHANGAA TUZO YA NOBEL SIJAPEWA MIMI. BADALA YAKE AKAPEWA ABIY AHMED WA ETHIOPIA Raisi wa Marekani Donal Trump ameonyesha kushangazwa na hatua ya kamati ya tuzo ya amani ya Nobel kumtea waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuwa mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2019 badala yake. Mwezi December, 2019 waziri mkuu wa Ethiopia alitangazwa mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kwa jitihada zake za kuleta amani na maridhiano nchini Ethiopia. Alipoingia madarakani mwaka 2018, Abiy alile...ta mabadiliko kadhaa ikiwemo kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa na wanaharakati, kuwakaribisha nyumbani wapinzani waliokimbilia nchi, kuwateua wanake katika nyadhifa za juu serikali, kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kuweza kufungua mpaka kati ya Ethiopia na Eritrea uliofungwa tangu mwaka 200. Akizungumza katika kampeni za uchaguzi mjini Ohio, Donald Trump amesema yeye alistahili kupata tuzo hiyo maana yeye ndiye aliyemsaidia Abiy Ahmed kuketa amani nchini Ethiopia na kuleta mapatano na Eritrea. " Ngoja niwaambie kuhusu Tuzo ya Nobel. Nimeiokoa hiyo nchi lakini cha ajabu nasikia tu kiongozi wa nchi hiyo ameshinda tuzo ya Nobel na aliyetoa msaada amesahaulika" alisema Trump. Unadhani nani alistahili kupata tuzo hiyo kati ya viongozi hao wawili?

WaterFront News 06.01.2021

Iran imetangaza zawadi Nono kiasi cha Dollar milioni 80 sawa na Shilingi bilioni 182 kwa mtu yeyote atakayewaletea kichwa cha Donald Trump raisi wa Marekani. Hii inafuatia mzozo ulioibuka baada ya Marekani kutekeleza mauaji ya generali Qassem Soleiman kamanda wa jeshi la wakurdi kwa tuhuma za ugaidi

WaterFront News 24.12.2020

Watu 51 wamefariki na wengine 213 kujeruhiwa vibaya katika mkanyagano nchini Iran wakati wa mazishi ya generali Qassem Soleiman aliyeuawa na Marekani Wiki iliyopita nchini Iraq.